ALAMA ZA SIKU YA KIYAMA

عودة للموسوعة

ALAMA ZA SIKU YA KIYAMA

Shukran zote ni za Muumba wa mbingu na ardhi Mola wa watu wote rehma na amani zimfikie Mtume Muhammad.

Katika khutba hii ya leo tutazungumzia kwa kina kumwamini Mwenyezi Mungu kikweli na siku ya mwisho pia tutahimizana kufanya vitendo vizuri na tutazindushana kukaribia siku ya kiama, vile vile nitahadharishe kutokana na fitna na njia za kujiepusha, na nimalizie kuzitaja alama za siku ya kiama.

Ama baada ya kumsifu Mwenyezi Muungu na kumtakia rehma na amani Mtume Muhammad. Ni vyema Muislamu yoyote popote alipo ajue kuwa nguzo za imani ni lazima na kuzifanyia vitendo vizuri. Katika nguzo za imani kuna kuamini siku ya kiama ambayo ni siku ya mwisho siku ya malipo na kabla siku hii haijafika kuna alama za kuonesha kwamba imeshakaribia. Na sio siri kwani zimesha dhihiri baadhi ya alama zake na haya ndio mazungumzo katika khutba yetu ya leo.

Enyi Waislamu watukufu! mazungumzo yetu ya leo yatahusu alama za kiama. Kwa hivyo ni vyema watu wajiandae na siku hiyo.

نطق تعالى : (فَهَلْ يَنْظُرُونَ إِلَّا السَّاعَةَ أَنْ تَأْتِيَهُمْ بَغْتَةً فَقَدْ جَاءَ أَشْرَاطُهَا فَأَنَّى لَهُمْ إِذَا جَاءَتْهُمْ ذِكْرَاهُمْ) [محمد: 18]

Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala): نطقب:Kwani wanangoja lingine ila kiama kiwajie? basi alama zake zimekwisha kuja, kutawafaa nini wakati kitakapowajia [ Muhammad : 18]. Ni lazima kwa kila muislamu kuamini siku ya mwisho alipe umuhimu mkubwa suala hili, kwani haikamiliki imani ya mtu mpaka aamini alama za kiama (kwani kuamini alama hizo ni katika kuamini siku ya kiama) ukizingatia kwamba Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) alizitaja alama hizi na hakitasimama kiama mpaka zitokee alama hizi. Swahaba Hudhaifa ibn Asiid radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: [ Tulikuwa tumekaa katika kivuli cha chumba cha Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) tukataja kiama na sauti zetu zikawa juu (mpaka Mtume akasikia) akasema : Hakitasimama au hakitakuwa kiama mpaka kupatikane kabla yake alama kumi].

Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) Amebainisha ya kwamba siku ya kiama haijulikani ni wakati gani na wala hakuna anayejua isipokuwa yeye peke yake. Na hakumhusisha yoyote kukijuwa kiama si Malaika aliyekurubishwa wala Mtume aliyetumilizwa na Mwenyezi Mungu. Pia imebainishwa kwamba kiama kimekaribia wakati wake kama zilivyoeleza Aya za Quran Tukufu na hadithi za Bwana Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam).

نطق تعالى) : يَسْأَلُونَكَ عَنِ السَّاعَةِ أَيَّانَ مُرْسَاهَا قُلْ إِنَّمَا عِلْمُهَا عِنْدَ رَبِّي لَا يُجَلِّيهَا لِوَقْتِهَا إِلَّا هُوَ ثَقُلَتْ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ لَا تَأْتِيكُمْ إِلَّا بَغْتَةً يَسْأَلُونَكَ كَأَنَّكَ حَفِيٌّ عَنْهَا قُلْ إِنَّمَا عِلْمُهَا عِنْدَ اللَّهِ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ) [الأعراف: 187] Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala): Amesema: نطقب:Wanakuuliza kuhusu kiama kitakuja lini? sema: ilimu yake iko kwa Mola wangu tu hakuna wa kudhihirisha wakati wake ila yeye. Imekuwa nzito mbingu na ardhi, hakita kuja kiama ila ghafla [Al-Araaf : 187].

ونطق) : يَسْأَلُكَ النَّاسُ عَنِ السَّاعَةِ قُلْ إِنَّمَا عِلْمُهَا عِنْدَ اللَّهِ وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّ السَّاعَةَ تَكُونُ قَرِيبًا) [الأحزاب: 63] Amesema Mola (Subhaanahu wa Taala): نطقب:Watu wanakuuliza kuhusu kiama kitakuja lini? sema: ilimu yake iko kwa Mola wangu tu. Na kipi kitakacho kujulisha lini kiama, pengine kiama kiko karibu [Al-Ahzab : 63]. Na pale Jibril alipomuuliza Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) kuhusu kiama Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) akajibu: [hakuwa mwenye kuulizwa ni mjuzi kuliko anayeuliza» Aya na hadithi za Mtume rehma na amani zimfikie zinazoshiria kwamba hakuna anayejuwa wakati wa kutokea kiama isipokuwa Mwenyezi Mungu]. Vile vile mitume waliobakia hawajui wakati gani kiama kitasimama.

Kwa kweli Mwenyezi Mungu amebainisha wazi kwamba kiama kimekaribia na vile vile Mtume wetu Muhammad rehma na amani zimfikie ameweka wazi katika hadithi zake kwamba kiama kimekaribia sana.

نطق تعالى :] (وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّ السَّاعَةَ تَكُونُ قَرِيبًا) [الأحزاب: 63]

Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) Amesema kwenye Qurani Tukufu: نطقب:Na kipi kitakujulisha lini kiama pengine kiko karibu [Al-Ahzab : 63].

نطق تعالى) : اقْتَرَبَ لِلنَّاسِ حِسَابُهُمْ وَهُمْ فِي غَفْلَةٍ مُعْرِضُونَ) [الأنبياء: 1]

Mola (Subhaanahu wa Taala) Amesema: نطقب:Imekaribia watu hisabu yao (ya kiama) nao wamo katika kughafilika na wanalipuuza [Al-Anbiya : 1].

Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) asema: [ Nimetumilizwa na kiama kama vidole viwili]. Akashiria vidole viwili cha kati na cha shahada.

Ndugu mnaonisikiliza napenda kuwabainishia vigawanyo vya alama za kiama. Kwa hakika alama za kiama zimegawanyika vigawanyo viwili.

Alama ndogo.

Alama kubwa.

Alama ndogo ni zinatangulia au zinazokuja kabla ya siku kiama kwa mda mrefu na zinazoeleka na zinaweza kudhihiri baadhi yake pamoja na alama kubwa au zikaja baada ya alama kubwa.

Ama alama kubwa ni mambo makubwa ambayo yatadhihiri karibu na kiama na huwa si ya kawaida kwa mfano kuja Dajjal na nyenginezo.

Na ukizingatia kudhihiri kwake zimegawanyika vigawanyo vitatu

Alama zilizodhihiri na kuweko

Alama zilizodhihiri na bado zinatokea

Alama ambazo hazijatokea mpaka sasa.

Alama Ndogo za Qiyama:-

Ndugu zangu Waislamu napenda kuzitaja alama ndogo za kiama nazo ni kama zifuatazo;

- Kutumilizwa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam). Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) amesema: [ Nimetumilizwa na kiama kama vidole viwili]. Akashiria vidole viwili cha kati na cha shahada.

- Kufa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) ni miongoni mwa alama ndogo za kiama, kwani ni ishara wazi ya kukatika wahyi kutoka mbinguni.

- Alama nyingine ya kiama ni kudhihiri fitna kubwa; itachanganyika haki na batili zitatikisika imani mpaka mtu ataamka asubuhi hali ya kuwa ni muislamu na atalala hali ya kuwa ni kafiri au atalala hali ya kuwa ni kafiri na ataamka hali ya kuwa ni muislamu.

Hii ni kuonesha kwamba mtu kuingia katika ukafiri ni wepesi kwa kule kuchanganyika haki na batili na ndio hali za zama zetu hizi, watu wamechanganyikiwa kiasi kwamba hawajui haki ni ipi na batili ni ipi. Na kila ikidhihiri fitna atasema haya ndio maangamivu yangu kisha itaondoka itakuja nyingine atasema muumini haya ndio maangamivu na na hazitawacha fitna kudhihiri kwa watu mpaka kiama kisimame. Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) amesema: [Hakika kabla ya kiama kutakuwa na fitna kama kipande cha usiku wa giza mtu ataamka muislamu na atalala kafiri na atalala kafiri na ataamka muislamu na aliyekaa ni bora kuliko aliyesimama na aliyesimama ni bora kuliko aliyetembea na anayetembea ni bora ni kuliko anayekwenda mbio].

Katika alama ndogo za kiama ni kudhihiri moto katika ardhi ya Hijazi na kupotea amana. Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [Hakitasimama kiama mpaka utoke moto katika ardhi ya Hijazi unatoa mwangaza moto huo kiasi utaona shingo za ngamia Basra]. Hakika moto huu umeshadhihiri katikati ya karne ya saba mwaka 654 hijria na ulikuwa mkubwa waliweza kuuona wanavyuoni wengi ambao waliokuwa zama hizo na waliokuja baada yao katika kuuelezea moto huo.

Vilevile kupotea amana ni katika alama za kiama watu kutotekeleza majukumu waliopewa na kutowajibika inavyotakiwa, Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) asema: [ Ikipotea amana ngojea kiama].

Katika alama za ndogo za kiama ni kuenea zinaa kiasi kwamba litakuwa jambo la kawaida na asiyejihusisha na jambo hilo watu. Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [Naapa kwa ambae nafsi yangu iko mkononi mwake hautamalizika umma huu mpaka asimame mwanamume na mwanamke na amlaze njiani afanye nae zinaa aseme mbora wao siku hiyo lau mtazunguka nyuma ya ukuta (mufanyie huko)].

Katika alama nyingine za kiama ni kuenea riba tukijua kuwa riba ni katika madhambi makubwa sana lakini namna itakavyoenea litakuwa jambo la kawaida, lakini watu hawajali na watajaza matumbo yao haramu.

نطق تعالى) : وَأَحَلَّ اللَّهُ الْبَيْعَ وَحَرَّمَ الرِّبَا( [البقرة: 275]

Mola (Subhaanahu wa Taala) Amesema: نطقب:Na Mwenyezi Mungu amehalalisha biashara na ameharamisha riba [Al-Baqara : 275]. Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) amesema: [ kabla ya kuja kiama kutadhhiri riba].

Miongoni mwa alama za kiama ni kudhihiri na kuenea muziki kwa wingi na watu watahalalisha miziki hiyo, Mtume ameeleza haya katika hadithi zake nyingi suala hili kwa hivyo inatakiwa Waislamu wachunge mipaka ya Mwenyezi Mungu kwa kuomba msamaha kwake na kutubia, kwani hali za wanaadamu ni mbaya na za kusikitisha sana. Huku tusisahau kupeana nasaha kwa kuamrishana mema na kukatazana yalio mabaya.

Miongoni mwa alama ndogo za kiama ni watu kujenga majumba makubwa na marefu tena kutoka kwa watu katika duni katika jamii kufikia kiwango cha utajiri na haya ni kwa mujibu wa maneno ya Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) alipotaja baadhi ya alama za kiama: [ Ni kuzaa mtumwa wa kike bwana wake na utaona watu wasiokuwa na viatu waliouchi, masikini, wachunga mbuzi wanashidana kurefusha majumba]. Na Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) amesema: [Hakitasimama kiama mpaka watu wajifakhiri kwa kujenga Misikiti].

Katika alama za kiama ni kukithiri uongo baina ya watu, watadanganyana kwa wingi huku tunajua kwamba uongo ni katika makosa makubwa Aliyoyakataza Mwenyezi Mungu katika Quran na vile vile Mtume rehma na amani zimfikie ameukataza uongo katia hadithi zake tukufu. Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) amesema katika hadithi yake: [ Hakitasimama kiama mpaka zidhihiri fitna, kukithiri uongo na kukaribiana masoko].

Vilevile hakitasimama kiama mpaka atamani aliye hai mauti kwa namna hali za watu zitakavyokuwa mbaya. Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) amesema: [ Hakitasimama kiama mpaka aende alie kaburini asimame aseme natamani mahali pako]. yaani atatamani alie hai afe yeye.

Kukaribiana masoko ni miongoni mwa dalili za kiama. Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) amesema: [ Hakitasimama kiama mpaka kukithiri uongo na kukaribiana masoko]. Hizi ndio miongoni mwa alama chache za kiama na ni vyema kwa muislamu yoyote azijue vizuri kwani akiziona huenda akajiandaa na siku ya mwisho kabla hajafikiwa na mauti kwa kufanya vitendo vizuri na kujiepusha na vitendo vibaya.

تاريخ النشر: 2020-06-09 07:08:22
التصنيفات:

مقالات أخرى من الموسوعة

سحابة الكلمات المفتاحية، مما يبحث عنه الزوار في كشاف:

آخر الأخبار حول العالم

الأرصاد: ارتفاع في درجات الحرارة نهارا بارد ليلا والصغرى في القاهرة 9

المصدر: بوابة أخبار اليوم - مصر التصنيف: سياسة
تاريخ الخبر: 2022-03-27 12:17:21
مستوى الصحة: 59% الأهمية: 61%

محافظ القاهرة يتفقد أعمال تطوير جامع الحاكم وشارع المعز

المصدر: بوابة أخبار اليوم - مصر التصنيف: سياسة
تاريخ الخبر: 2022-03-27 12:17:20
مستوى الصحة: 52% الأهمية: 58%

الاستعانة بالصلاة

المصدر: الجماعة.نت - المغرب التصنيف: سياسة
تاريخ الخبر: 2022-03-27 12:20:14
مستوى الصحة: 58% الأهمية: 66%

محمد بن راشد يستقبل رئيس حكومة إقليم كردستان العراق

المصدر: الإمارات اليوم - الإمارات التصنيف: مجتمع
تاريخ الخبر: 2022-03-27 12:17:46
مستوى الصحة: 47% الأهمية: 50%

مجلس الشيوخ يحيل 10 تقارير للجان النوعية للحكومة

المصدر: بوابة أخبار اليوم - مصر التصنيف: سياسة
تاريخ الخبر: 2022-03-27 12:17:22
مستوى الصحة: 53% الأهمية: 57%

مهاجم على طاولة نادي ليفربول لتعويض محمد صلاح "مجاناً"

المصدر: الإمارات اليوم - الإمارات التصنيف: مجتمع
تاريخ الخبر: 2022-03-27 12:17:47
مستوى الصحة: 53% الأهمية: 53%

الركراكي: هناك من حذرني من التعاقد مع الوداد بسبب الناصري

المصدر: راديو مارس - المغرب التصنيف: رياضة
تاريخ الخبر: 2022-03-27 12:17:39
مستوى الصحة: 51% الأهمية: 57%

رئيس مجلس الشيوخ يفتتح أعمال الجلسة العامة

المصدر: بوابة أخبار اليوم - مصر التصنيف: سياسة
تاريخ الخبر: 2022-03-27 12:17:20
مستوى الصحة: 58% الأهمية: 68%

توقعات أحوال الطقس اليوم الأحد

المصدر: تيل كيل عربي - المغرب التصنيف: سياسة
تاريخ الخبر: 2022-03-27 12:17:50
مستوى الصحة: 58% الأهمية: 51%

تحميل تطبيق المنصة العربية