Athari ya kusuhubiana na rafiki mwema
Matunda ya kusuhubiana na rafiki mwema kuongoka kwa mtu mmoja ni kuongoka kwa jamii na kuongoka kwa jamii ndio sababu ya kupata baraka inayotoka mbinguni na ardhini. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):
نطق تعالى) : وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْقُرَى آَمَنُوا وَاتَّقَوْا لَفَتَحْنَا عَلَيْهِمْ بَرَكَاتٍ مِنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ وَلَكِنْ كَذَّبُوا فَأَخَذْنَاهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ ) [الأعراف: 96]
نطقب:Na lau kama watu wa miji wangaliamini na kuogopa, kwa yakini tungaliwafungulia baraka za mbingu na ardhi. Lakini walikadhibisha; tukawapatiliza kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyachuma. Watu wa peponi wote ni marafiki wema.
Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):
نطق تعالى: (إِنَّ الَّذِينَ آَمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ كَانَتْ لَهُمْ جَنَّاتُ الْفِرْدَوْسِ نُزُلًا ) [الكهف: 107]
نطقب:Kwa yakini walioamini na kufanya vitendo vizuri, makazi yao yatakuwa hizo za Firdaws.
Na Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) :
وقوله تعالى: (وَنَزَعْنَا مَا فِي صُدُورِهِمْ مِنْ غِلٍّ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهِمُ الْأَنْهَارُ) [الأعراف: 43] نطقب:Na tutaiondoa bughudha vifuani mwao (wawe wanapendana wote kweli kweli) mbele yao iwe inapita mito. Wema waliotangulia ni mfano bora wa kusuhubiana. Pindi Salman alipomtembelea Abu Dardai akamuona Mama Dardai nae akamuuliza kuhusu Abu Dardai nae akamjibu kuwa ametoka na muda si mrefu atarudi. Ummu Dardai akamjulisha Salman tabia ya Abu Dardai ya kuachana na dunia na kutoangalia watu wake. Pindi aliporudi Abu Dardai mazungumzo yao yalikuwa kama hivi ifuatavyo:
Abu Dardai alimwambia Salama: Kula chakula hichi mimi nimefunga. Salman akajibu sili chakula hichi mpaka ule wewe. Abu Dardai akala chakula hicho. Ilipofika usiku Abu Dardai alitaka kusimama (Qiyamulail). Salman akamwambia: lala. Abu Dardai akalala, jambo hilo likaendelea mara mbili tatu ilipofika usiku wa mwisho Salman akasema: amka sasa Mola wako na nafsi yako pia ina haki kwako. Vile vile pia mke wako ana haki kwako, ipe kila haki haki yake. Aliposikia Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) akasema: “ Amesema kweli Salman.” Tazama vipi waja wema wanavyosaidiana kwa amali njema na kumcha Mwenyezi Mungu.
Mfano wa rafiki muovu na mwisho wake, Abu Talib alipokuwa anafikiwa na mauti Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) alimtembelea na hapo alikuwepo Abu Jahal na ‘Abdallah Ibn Abi Umaya Ibn Mughaira. Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) akasema kumuambia Abu Talib aseme “Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu “ neno ambalo litakutolea hoja mbele ya Mwenyezi Mungu, akasema Abu Jahal na ‘Abdillah Ibn Abi Ummayah unaipa nyongo mila ya AbdulMutwalib. Hakuacha Mtume wa Mwenyezi Mungu kumkariria, na wao pia wakikariri “Unaipa nyongo mila ya AbdulMutwalib” mwishowe akasema yeye yuko katika mila ya AbdulMutwalib.
Enyi baba zangu nyote ni wachunga na kila mmoja ataulizwa kwa kile anacho kichunga. Itakuwa ni khiana baba kuwaacha watoto wake bila ya kuwauliza wanakwenda wapi, hali ya siku hizi hawaulizi wanapokwenda au walikuwa pamoja na nani? Na wapi wamelala? Wala hajui baba kwamba mtoto wake alikuwa na rafiki wa kishetani wakimuharibu dini, akili yake na uislamu wake. Tahadhari na marafiki waovu, na ni juu ya barobaro kuchagua rafiki mwema ambao watakaomsaidia katika haki na kumjuza.
Mwisho
Ndugu katika Imani, ni muhimu sana kuchagua rafiki mwema ambaye atakusaidia katika kufanya mambo ya kheri. Pindi unapo sahau anakukumbusha na ukikosea anakunasihi kwa njia mzuri.
Ewe Mwenyezi Mungu turuzuku rafiki wema na utuepushie na rafiki waovu, uturuzuku rafiki wema ambao watatusaidia katika kukushukuru na kukutaja na kukuabudu na uturuzuku kusuhubiana na Mtume wako.